Diamond akiwakabidhi washindi zawadi zao.
Meneja Masoko, Darsh Pandit, akizungumza jambo.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Bardesh Pandit, akizungumza na wanahabari.
Mwanamuziki Diamond ambaye ni balozi wa kampuni ya RedGold akizungumza kuhusu bidhaa ya RedGold.
MWANAMUZIKI wa Bongo Flava, Nassib Abdul ‘Diamond’, ambaye sasa ni balozi wa kampuni ya RedGold nchini leo amewakabidhi zawadi washindi waliokuwa wakishiriki katika droo ya ‘Shinda mamilioni na RedGold katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Crystal uliopo katika hoteli ya Blue Pearl ya Ubungo jijini Dar.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, Darsh Pandit, alisema ili kushiriki shindano hilo mshiriki anatakiwa kununua Tomato Sauce au Chilli Sauce kisha atatuma namba iliyo ndani ya kizibo ili kuwa mshindi katika ambayo huchezeshwa kila Ijumaa kupitia radio ya Clouds na EfM ambapo mteja akifungua chupa ya RedGold anatuma namba za kizibo kwa sms kwenye namba 15729 au 0688808888.
NA IMELDA MTEMA/GPL







