Mke wa Marehemu Makongoro Oging’ aitwaye, Naza (kushoto) akiwa na baadhi ya watoto wake, Baraka (katikati) na Leah Makongoro.

Mtoto wa Marehemu Makongoro, Leah Makongoro (kulia) akilia kwa uchungu.

Waombolezaji wakiwa msibani hapo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (katikati) akiwa na waombolezaji msibani kwa Makongoro Tabata – Magengeni, Dar.

Wafanyakazi wa Global Publishers wakiongozwa na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul (kulia) wakiwa katika maombolezo nyumbani kwa marehemu Makongoro.

Waombolezaji wakiwa msibani hapo.

Waombolezaji wakiwemo wafanyakazi wa Global wakifanya shughuli mbalimbali msibani hapo.

Mhariri Kiongozi wa Global,Oscar Ndauka (wa pili kulia) akiwa na waombolezaji msibani hapo.

Mkurugenzi Shigongo akijadili jambo na Mhariri Mwandamizi wa Global, Elvan Stambuli msibani hapo.
Pichani juu ni taswira kutoka msibani kwa aliyekuwa mwandishi wa habari mwandamizi wa Gazeti la Uwazi la Kampuni ya Global Publishers Ltd, Makongoro Oging’ aliyefariki dunia Mei 21 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu Makongoro umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana Jijini Dar ambapo kwa taarifa za awali unatarajiwa kusafirishwa kwenda kijijini kwao Marasibora Wilayani Tarime, Mkoani Mara kwa ajili ya mazishi Alhamisi.
Kabla ya kusafirishwa mwili huo waombolezaji wanaendelea kutoa pole kwa wafiwa nyumbani kwake Tabata Magengeni, Dar.
