×

Sheta: namjua itaifunika Shikorobo

shettaWilbert Molandi, Dar ess Salaam
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Sheta anaamini kuwa songi lake jipya la Namjua litaifunika ngoma yake ya Shikorobo aliyomshirikisha Kcee kutoka Nigeria. Kauli hiyo, ameitoa ikiwa ni siku chache tangu aitambulishe audio ya ngoma hiyo na kichupa chake kwenye vituo vya radio na televisheni.
Sheta alisema namjua itaifunika Shikorobo Jumatano kuwa, Namjua itafunika kutokana na jinsi wimbo huo ulivyopokelewa na mashabiki wake tangu auachie.
“Awali nilipoitambulisha rasmi Namjua, wengi walisema haitaweza kuifikia Shikorobo, lakini kadiri siku zinavyokwenda ninaona kabisa Namjua itafunika siku za mbele.
“Kwa sababu hata ukiangalia kwenye mitandao, mashabiki wengi wanaipongeza sana Namjua, hivyo ninapata matumaini nyimbo hiyo kufanya vyema kwenye radio na televisheni,” alisema Sheta

Leave a Comment