×

Shinda Nyumba Droo Ndogo… Washindi Kukabidhiwa Zawadi zao Leo

DROO NDOGO YA SHINDA NYUMBA (6)

MARA baada ya kufanyika kwa droo ndogo ya mwisho ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers, wiki iliyopita washindi waliopatikana wa pikipiki, vyombo vya jikoni, mashuka, simu ya kisasa na ving’amuzi wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao leo (Jumatano).

SHINDA NYUMBA (22)Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko, Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda alisema kuwa washindi hao ni Akani Msemwa kutoka Mbalizi, Mbeya aliyejishindia seti ya vyombo vya jikoni, Richard Mauga kutoka Dar aliyejishindia simu ya kisasa, Maria Mwakale aliyejishindia mashuka, Evans William wa Dar aliyejishindia pikipiki aina ya Skymark pamoja na washindi watano waliojishindia kila mmoja king’amuzi cha Ting,” alisema Mkanda.

Droo kubwa inatarajiwa kufanyika mwezi ujao ambapo mshindi atakabidhiwa nyumba ya kisasa yenye samani ndani iliyopo, Salasala jijini Dar.

Leave a Comment