×

Kuwa mwerevu na huduma ya Global Breaking News

breakingKuwa mwerevu na huduma ya Global Breaking News

  • Unajua yote yanayojiri hata usipotoka nje!
  • Unakuwa wa kwanza kupata habari kabla ya TV, magazeti
  • Gharama yake kwa siku ni karibu na bure!

M

AISHA yanakwenda yakibadilika kwa kasi ya ajabu kwelikweli, hasa katika teknolojia. Nakumbuka zamani, wakati huo nikiishi Singida mjini, magazeti yalikuwa yakija siku tatu baadaye, yaani kwa mfano, gazeti la leo Ijumaa, unalisoma Jumatatu, tena huku ukifurahia kupata gazeti la ‘leo’.

Ukiondoa magazeti, taarifa nyingine muhimu za dunia na nchi, zilipatikana kupitia redio, (RTD) wakati huo, ndiyo maana vipindi na watangazaji waliweza kufahamika nchi nzima. Hakukuwa na televisheni wala internet.

Lakini leo, miundombinu ikiwa imeboreshwa, siyo tu magazeti yanapatikana leoleo, lakini pia yako mengi na vituo vya redio ni vingi kiasi vingine havifahamiki na watangazaji wake hawajulikani, ukiacha vichache, hasa vya jijini Dar es Salaam.

Pia kuna vituo lukuki vya televisheni, achilia mbali mitandao ya kijamii inayopatikana katika internet, kiasi kwamba ni rahisi kwa mtu kupata habari za ndani na nje kwa wakati muafaka. Ujio wa simu za mikononi, hasa za kisasa, umeongeza urahisi wa upatikanaji wa habari.

Global publishers, kwa kutambua umuhimu wa upashanaji habari, hasa kwa muda na wakati, imekuja na namna mpya ya kuhakikisha wasomaji wa magazeti yake, wanakuwa wa kwanza kupata taarifa zote muhimu, za ndani na nje ya nchi.

Huduma hii inayojulikana kama Global Breaking News itamuwezesha msomaji kupata habari za muda huo huo kupitia simu yake ya mkononi. Yaani, msomaji popote alipo Tanzania atapata habari na matukio muhimu yanayotokea muda huo huo.

Anachotakiwa kufanya msomaji, ambaye anatumia Mtandao wa Vodacom ni kutuma neno GLOBAL kwenda nambari 15778 ili kujiunga na huduma hii. Na kwa kupata taarifa zote hizo, mtumiaji wa huduma hii atakatwa shilingi mia moja tu kwa siku!

Yes, kwa shilingi mia moja, utaweza kupata habari na matukio yanayotokea muda huo huo, kutoka popote ulipo kupitia simu yako ya mkononi. Kwa mfano, inapotokea ajali mbaya ya gari, ndege au matukio makubwa ya kidunia, unakuwa wa kwanza kupata habari kabla hazijatangazwa na vyombo vingine vya habari.

Hii ni huduma ya kisasa yenye gharama nafuu zaidi kuliko kawaida katika kupata habari. Hakuna gharama katika kujiunga.

Maana nyingine ni kuwa hata ukiamua kulala ndani kutwa nzima, ukiwa shambani kwako, ukiwa mgonjwa, ukiwa safarini, kupitia simu yako, Global Breaking News itakupatia kila kinachojiri duniani kwa wakati muafaka.

Kwa urahisi wa kujiunga na gharama ilivyo nafuu, ni kujiweka nyuma wewe mwenyewe katika kuitambua dunia inayokimbia na matukio yanayotokea kila pembe ya sayari hii!

Leave a Comment