MSANII anayeuza ‘nyago’ kwenye kiwanda cha Filamu Bongo aliyeamua kugeukia kwenye Muziki wa Injili pia, Gift George ‘Gift Mwamba’ amefunguka kuwa baada ya kutoa Ngoma za Nimerudi na Uwepo wa Mungu alizofanyia katika studio tofauti hivi karibuni anategemea kuachia wimbo mpya uitwao Ndoa.
Akichonga na Uwazi Showbiz, Gift alisema kuwa ameamua kutoa wimbo huo ili kuwapa elimu watu ambao wako kwenye ndoa, lakini pia kuwasisitiza kumtegemea Mungu kuiongoza ndoa yao.
“Wimbo wa Ndoa utawafaa sana watu ambao wako kwenye ndoa, una mafundisho mengi na hakika ninautegemea kufanya vizuri katika tasnia ya Muziki wa Injili,” alisema Gift.
