NEW YORK, MAREKANI
KWISHNEI! Baada ya kuishi kwa muda wa miezi 15 kama wapenzi, hatimaye staa wa Muziki wa Pop, Tylor Swift amebwagana na mpenzi wake ambaye ni DJ, Calvin Harris.
Awali kabla ya kuachana, ilidaiwa kuwa Calvin alionekana akiwa katika maduka ya kuuzia vito vya thamani akichagua pete kwa ajili ya kumchumbia Tylor lakini jambo hilo alikuja kulikanusha.
Hivi karibuni Jarida la People la Marekani liliripoti kuwa Calvin alifikia hatua ya kumuacha Tylor huku sababu zikifichwa.
Napo kupitia ukurasa wa Twitter wa Calvin, aliwathibitishia mashabiki wake kuwa hayupo kwenye uhusiano wa kimapenzi tena ambapo aliandika;
“Ukweli uliobaki katika uhusiano wangu ni kwamba umefikia tamati, itabaki kuwa tulikuwa na mapenzi kwa kiasi kikubwa na heshima.”
Wapenzi wengine aliowahi kuwa nao Tylor kabla ya Calvin ni Joe Jonas (2008), Lucas Till (2009), John Mayer (2009), Taylor Lautner (2010), Jake Gyllenhaal (2010), Conor Kennedy (2012) pamoja na Harry Styles (2012 –2013).
