Kanisa la Sinza Christian Center limetupiwa nje vyombo vyake nje kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutokana na kanisa hilo kudaiwa deni la zaidi ya Sh. milioni 100. Aliyetekeleza agizo hilo leo ni dalali aliyepewa tenda hiyo Bw. Joshua ambaye aliteuliwa na Mahakama na jmiliki wa jengo hilo Bw. Prosper Rwendera.
Akizungumza wakati wa hamisha hamisha hiyo, mke wa mmiliki wa jengo hilo, Bi. Patricia Prosper alisema; “Huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu.”
Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.
Viti vyote vikiwa vimetolewa nje.
Vifaa vikiwa vimetolewa nje.
Magari yakiwa yanatolewa nje
Vitu vikiwa nje ya Jengo hilo ambapo mpaka sasa kuna sinto fahamu vinapelekwa wapi.
Vikombe nje.
Wametoa vitu vyote.
Magodoro na vitanda vyote nje.
Baadhi ya Magari yaliyotolewa katika Jengo hilo ambapo hapo awali ilikuwa ni Kanisa
Kushoto kwa mbali ni Mke wa Miiliki wa Jengo hilo Bi. Patricia Prosper akiendelea na majukumu huku pembeni vijana wakipata maelekezo ya kuendelea kutoa vitu.


