×

Uche agonga 30, awashangaza mashabiki

Uche-Ogbodo-October-2013-BellaNaija

Andrew Carlos

STAA mkongwe wa fi lamu Nollywood, Uche Ogbodo wiki iliyopita alitimiza miaka 30 na katika kusherehekea aliwashangaza mashabiki wake wengi baada ya kutokelezea akiwa ‘close’ na mchumba wake mpya ambaye hakujulikana jina.

Nollywood 1Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Uche alitupia picha za bethidei yake zikimuonesha akila bata na mchumba wake
pamoja na marafi ki zake katika Ukumbi wa Tribeca uliopo Lagos, Nigeria ambapo muda mwingi walionekana wakipigana mabusu huku wakiwa` ‘zero distance.’

376Mwaka jana, Uche alitemana na mumewe, Ato Ubby ambapo chanzo cha kumtema ilidaiwa ni kwa sababu alikuwa na tatizo la uvimbe kwenye kichwa.

Leave a Comment