Stori: GABRIEL NG’OSHA, WIKIENDA
DAR ES SALAAM: Zikiwa zimebaki siku tatu sawa na saa 72 kabla ya kufungiwa kwa simu feki nchini Tanzania, Alhamisi wiki hii na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA -Tanzania Communication Regulation Authority), inakadiriwa simu za watu zaidi ya milioni 6 zitakwenda na maji.
Imeelezwa kuwa unapozungumzia watu zaidi ya milioni sita maana yake yake ni zaidi ya simu feki milioni sita kwani kuna wengine wana simu zaidi ya moja.
Kufuatia hali hiyo, Wikienda lilizungumza na watu mbalimbali akiwemo Mbuge wa Mtera (CCM) mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde ambaye alisema serikali imefanya makosa kama ilitaka udhibiti wa vitu feki basi ingedhibiti kwenye uingiaji na siyo kujitwisha mzigo kwa dhambi ya kuwasababishia Watanzania kutumia vitu feki.
“Kiukweli serikali ilichofanya ilifikiri ni kama kuhamisha mfumo wa mawasiliano wa analojia kwenda digitali lakini imekosea sana, imejitwisha mzigo mkubwa wa dhambi, kwanza serikali itapoteza mapato lakini hata hizo kampuni na hata Watanzania wenyewe zaidi ya milioni kama sita watapoteza mawasiliano,’’ alisema Lusinde.
TCRA iliahidi kuzifungia simu zote feki ifikapo Juni 16, mwaka huu na hakutakuwa na muda wa nyongeza.
mimi naishangaa sana serikali yetu kwa kuchachamaa na kukomaa kuhusu simu feki,na kupigia kifua mpaka azma ikatekelezwa,lakini hapo hapo wamesahau kama kuna ktu ambacho ni muhimu zaidi kwa binaadam na watanzania kwa ujumla,kitu ambacho si chengine bali ni afya,,sasa mbona hawazionei huruma afya za wananchi wao na badala yake kunaingizwa vyakula matunda na mengi mengineyo na wao wamelikalia kimya jambo hili?
nayo pia ni feki lakini hili limekaliwa kimya???