KWAKO mkongwe wa Hip Hop Bongo, Juma Mchopanga ‘Jay Mo’. Habari za siku ndugu yangu. Maisha yanakwenda? Kitambo sana sijakutia machoni lakini kupitia wimbo wako mpya wa Pesa ya Madafu naamini Mungu ni mwema, anaendelea kukupigania. Ukitaka kujua afya ya mimi nduguyo, sijambo. Namshukuru Mungu, naendelea vizuri. Napambana kama kawa kwenye ulimwengu wetu wa habari.
Tunapambana kuhakikisha Watanzania wanahabarika, wanaburudika na kuelimika pia. Madhumuni ya kukuandikia
barua hii si mengine zaidi ya kutaka kujua nini kinachokusibu hadi ututese sisi mashabiki wako. Sikia Jay Mo, unatukosea sana sisi mashabiki wako maana unashindwa kukata kiu yetu kutokana na ukimya wako kwenye gemu.
Unakaa muda mrefu sana pasipo sisi kupata kitu kipya kutoka kwako. Haimaanishi kwamba kuwa na utaratibu wa kutoa wimbo baada ya muda mrefu kupita ni mbaya, lakini una kila sababu ya kukaa karibu na mashibiki wako.
Ninasema hivyo kwa sababu mimi nimekujua kwa sababu ya muziki. Tumekuwa tukizungumza lugha moja kupitia muziki.
Tangu enzi zile za Mvua na Jua, Stori Tatu, Maisha ya Boarding, Cheza Kwa Step na nyingine kibao, ulikuwa karibu nami. Ulijitengenezea heshima kubwa ya utunzi. Nyimbo zako zilikuwa zinabeba ujumbe mzito na vina. Tulikuwa
tunakaa muda mfupi tunasikia wa barua yangu, kwa nini uwe unakaa kimya wakati uwezo unao. Wewe umewashawishi vijana wengi sana kufanya huu muziki nchini. Wewe si wa kuwaacha kina FA na AY waendelee kutusua ilhali una uwezo mkubwa.
Mashabiki wako tunataka vitu vizuri kutoka kwako. Tunataka ladha yako iendelee kusikika katika spika za redio
na kukutazama katika runinga mbalimbali. Tunataka kuona mafanikio yako. Tunataka kusikia kwamba kutokana na
ukongwe wako katika muziki, umepiga hatua kubwa ya kimaendeleo.
Sina maana kwamba huna mafanikio, hapana, yapo lakini pengine ungeendelea kusikika kwa nyimbo kila wakati kila
mtu angezidi kuvutika na wewe. umefanya kitu. Umeachia wimbo mpya au pengine hata habari zako zinazungumzwa
kwenye vyombo vya habari. Lakini hiyo ilikata ghafla.
Badala yake kukawa na ukimya wa muda mrefu. Kikapita kimya kirefu tena hadi juzikati nilipokusikia umeibuika na Pesa ya Madafu. Kwanza nikupongeze ndugu yangu, Jay Mo wa Pesa ya Madafu ni mwingine sana. Hujapoteza uhalisia wako lakini kuna vitu fulani ambavyo umeviongeza katika namna yako ya ‘kuchana’ lakini kwa ujumla wake
wimbo umekuwa mkali balaa. Kama hiyo haitoshi, video yake nayo imetendewa haki. Mandhari nzuri, Kwetu Studio wametisha sana. Hapo ndipo kwenye msingi
Bado vijana wangeendelea kuguswa na uwezo wako na pengine wangependa kuwa kama wewe. Wewe unapaswa kuwa na heshima kama walizonazo kina Profesa Jay, Sugu na wengine ambao tunawaona kwa sasa wana nafasi za juu kutokana na muziki. Mimi natamani utamu ule wa Wateule urudi. Niwasikie kina Mchizi Mox, Jafarai na Solo Thang!
Mimi ujio wako mpya nimeukubali, nikusihi ndugu yangu usituangushe. Fanya kweli. Anzia hapo, weka juhudi zaidi na tuwe tunakusikia mara kwa mara.
Mimi ni nduguyo;
………………………
Erick Evarist
