Lamar Odom na mkewe, Khloe Kardashian.
Miezi kadhaa baada ya kunusurika kupoteza maisha kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kujiovadozi madawa ya kulevya na kusababisha alazwe hospitali kwa muda mrefu, mcheza kikapu mstaafu aliyejipatia umaarufu mkubwa akiwa na timu ya Los Angeles Lakers, Lamar Odom anatajwa kurudia tena kula unga, jambo lililosababisha mkewe, Khloe Kardashian kuendelea kushikilia msimamo wake wa kudai talaka.
Katika tukio la hivi karibuni, Odom alinaswa akiwa amelewa tilalila, huku akiendelea kunywa pombe kwenye baa maarufu ya Los Angeles Beverly Center Mall ambapo wachunguzi wa mambo, walieleza kuwa kwa jinsi alivyokuwa amelewa, ilikuwa dhahiri kwamba alijidunga kwanza madawa kabla ya kuanza kunywa pombe.
Madai hayo ya kurudia tena madawa, yamesababisha mkewe Khloe ambaye kwa kiasi f ulani alishaanza kulegeza msimamo wake wa kutengana na kuanza kurudisha mapenzi kwa Lamar, kutangaza kwa mara nyingine kwamba kamwe hawezi kurudiana tena na Lamar mpaka atakapoacha kabisa matumizi ya madawa ya kulevya.