×

Mohammed Morsi wa Misri Ahukumiwa Kifungo cha Maisha

morsi

Mohammed Morsi.

MAHAKAMA nchini Misri imemhukumu kifungo cha maisha jela aliyekuwa rais wa Misri, Mohammed Morsi baada ya kukamilika kwa kesi yake ya upelelezi.

Morsi ni miongoni mwa washtakiwa wanaoshutumiwa kwa kutoa nakala za siri kwa taifa la Qatar.

Wakili wa Morsi ameeleza kuwa aliachiwa huru kwa upelelezi lakini akapewa hukumu hiyo kutokana na kuliongoza kundi haramu.

Mohammed

Hata hivyo kiongozi huyo wa zamani ana uwezo wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama uliotolewa wakati ambapo sekta ya mahakama ya Misri inaendelea kukosolewa na makundi ya wanaharakati duniani.

Morsi alikuwa rais wa tano wa Misri aliyeliongoza taifa hilo kuanzia Juni 30, 2012 mpaka Julai 3, 2013 alipoondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Genarali Abdel Fattah el-Sisi.

Leave a Comment