×

Wiki Ya Miujiza Imewadia!

9.Hamisi Shabani (kulia) akishiriki kujaza kuponi yake ili kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba. Na Mwandishi Wetu, Risasi Mchanganyiko

KAMA kuna kitu mwanafunzi wa ngazi yoyote huwa anakisubiri kwa hamu kubwa, basi huwa ni matokeo ya mitihani aliyofanya, hasa ile ya kumaliza elimu yake, kwani hiyo huamua hatima ya maisha yake, kama atapenya kidato cha pili, nne, sita au hata chuo kikuu.

Hata awe hakuwa mtu anayejali masomo kiasi gani, siku matokeo yakitoka, lazima atachungulia kuona alivyofanya na wengi hujisikia vibaya wanapopata matokeo ambayo hawakuyatarajia.

NYUMBA (17)Kinachotokea kwa wasomaji wa Magazeti ya Ijumaa, Championi, Risasi, Amani, Uwazi na Ijumaa Wikienda ni kama wanafunzi ambao sasa wapo chumba cha mitihani, wanafanya majumuisho ya kuponi zao walizojipatia kwa ajili ya droo kubwa zaidi kuwahi kufanywa na chombo cha habari nchini Tanzania, ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

Droo hii ilianza yapata miezi sita iliyopita, lakini katika hali inayotia faraja, hatimaye kilele chake kimewadia, kwani hadi unaposoma gazeti hili, zimebakia siku saba tu kabla ya kufanyika bahati nasibu hiyo ili mtu mmoja ambaye huenda ni wewe msomaji, ajipatie zawadi hii kubwa, ambayo hakika ni kama imetoka kwa Mungu.

Katika muda huu, lolote linaweza kutokea la kukuwezesha wewe kuibuka mshindi, kwani kama ulikuwa hujawahi kukata kuponi yako kutoka mojawapo ya magazeti hayo, muda bado upo. Fanya hivyo haraka na kwa uhakika zaidi.

Kama ulishakata kuponi zako, unachotakiwa kufanya ni kuzihifadhi vizuri, kwa sababu kila kipande cha karatasi chenye kuponi, kinaweza kubadili maisha yako. Unashauriwa kununua kuponi zaidi ili kupanua wigo wako wa ushindi.

Siku ile ya Juni 30, mwaka huu, ndiyo siku ambayo matokeo ya wanafunzi wote walioshiriki mtihani huu yatatolewa. Tofauti na mitihani ya darasani, huu wala hauna maswali magumu yanayohitaji ulaze miguu kwenye ndoo ya maji ili kujisomea!

Ni mtihani rahisi kupindukia kwa sababu mshindi anatakiwa kufanya kitu kimoja tu, ambacho ni kununua mojawapo ya gazeti za Global Publishers ili upate kuponi yako na kuipeleka kwa wakala wao au kwenda mwenyewe ofisini kwao Bamaga Mwenge ili ihifadhiwe kusubiri siku ya ‘shoo’.

Kitu kingine cha kuzingatia ni kuwa Mwenyezi Mungu aliiumba kila siku na bahati yake, sasa kama ulishanunua kuponi kadhaa huko nyuma halafu ‘ume-relax’ kwa kujua zinatosha, unakosea, huenda kuponi ya leo ndiyo imebeba mzigo!

Kwa hiyo, kama una mia tano nunua gazeti la siku hiyo liwe ni Championi, Ijumaa Wikienda, Ijumaa (hili sasa utalipata kwa buku), Risasi, Uwazi au Amani halafu jifunge na Mungu wako kusubiri muujiza huu ambao lazima utatokea.

Leave a Comment