×

Iggy: Siolewi na mwanaume nisiyemuamini!

nicky-young-iggy-azalea-won-heart-gty-ftr

ZIKIWA zimepita siku kadhaa tangu rapa wa kike kutoka Australia, Iggy Azalea atemane na mchumba wake ambaye ni mkali wa mpira wa kikapu anayechezea LA Lakers, Nick Young, bi’dada huyo amefunguka kuwa kamwe hawezi kuruhusu kuolewa na mwanaume ambaye hamuamini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Iggy (26) ambaye alivalishwa pete na staa huyo Juni, 2015 kisha tetesi za kuoana zikivuma, aliandika;

“Nampenda sana Nick, nilijitahidi nakujitahidi kuujenga uaminifu upya kwake, imekuwa tofauti wiki zilizopita. Namtakia maisha mema. Si kitu rahisi kumuacha mtu uliye na mipango naye lakini mipango inaweza kuandikwa upya lakini kwangu kurasa ni nyeupe nimeshafuta.”

Iggy na Nick walianzisha uhusiano miaka miwili iliyopita ambapo mwaka jana walivalishana pete lakini hivi karibuni walikuja kuachana huku Iggy akiweka hadharani sababu ya kuachana ni kusalitiwa.

Leave a Comment