×

Baada ya kupata ajali… Wasanii wamfanyia dua maalum Dotnata

DotnataStori: Gladness Mallya

MSANII mkongwe kwenye gemu la filamu Bongo, Illuminata Poshi ‘Dotnata’ hivi karibuni alifanyiwa dua maalum na wasanii baada ya kuwaalika nyumbani kwake Ubungo, Dar kwa ajili ya futari.

Dotnata aliyepata ajali ya kuanguka na kuvunjika mfupa wa paja, aliwaalika mastaa mbalimbali wa filamu ambao walipomaliza kufuturu walimuombea dua maalum huku wakimshukuru Mungu kwa kuwa anaendelea vizuri.

“Nimefurahi sana wasanii kuitikia wito wangu, kufuturisha siyo utajiri ni moyo tu jamani, nimefarijika sana kwa dua ambayo wenzangu wameniombea, kubwa nawaomba tupendane ili tuweze kuipeleka mbele sanaa ya filamu kwani kwa sasa hali ni mbaya,” alisema Dotnata.

1 Comment

Leave a Comment