Mika Samson (kulia) mkazi wa Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar akielekezwa na Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda, namna ya kujaza kuponi kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.







BAHATI nasibu ya ‘Shinda Nyumba’ ikiwa imebakiza siku chache tu kuchezeshwa, Jana Ijumaa promosheni ya shindano hilo iliwafikia wakazi wa Kibamba na maeneo mengine jijini Dar waliojitokeza kwenye gari la matangazo walipochangamkia kununua Toleo Jipya la gazeti la Ijumaa na kushiriki kujaza kuponi za bahati nasibu hiyo.
Bahati nasibu hiyo inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Championi, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.
Akizungumza na wakazi eneo hilo, Ofisa Masoko wa Global Publishers,Yohana Mkanda alisema kuwa zimebaki siku nne hivyo wachangamkie fursa hiyo kwani nyumba hiyo inaweza kupata mshindi miongoni mwao.
Katika uhamasishaji huo, Yohana Mkanda alirudia wito wake kwamba: “Siku zimebaki nne nunueni magazeti ya Global mengi na mjaze kuponi ili kujiongezea nafasi ya kushinda nyumba kwani unaweza kuwa wewe au yule na kugeuka baba au mama mwenye nyumba! Hivyo, fursa ndiyo hii, bahati humjia mtu yeyote, kwa hiyo nunua magazeti yetu pendwa yaliyojaa bahati na kila namna kila wakati. Kazi kwako, nyumba ndiyo hiyoo…!!!”
NA DENIS MTIMA/GPL

