PRODYUZA na muimbaji wa nyimbo za Injili, Goodluck Gozbert ‘Lolly Pop’ amezima tetesi zilizozagaa kuwa wimbo mpya wa Bernad Paul ‘Ben Pol’ wa Moyo Mashine ulikuwa umeandikwa maalum kwa msanii, Baraka Andrew ‘Barakah Da Prince’ kuwa si kweli.
Akigonga stori mbili-tatu na mtandao huu, Lolly Pop ambaye amehusika katika kumwandikia mashairi nyimbo karibu zote za Barakah alisema kuwa Wimbo wa Moyo Mashine aliuandika mwaka jana na ulikuwa mahususi kwa Ben Pol.
“Si kweli kama nimempa wimbo Ben Pol badala ya Barakah. Kwanza Moyo Mashine imepikwa na maprodyuza watatu yaani mimi Kidboy na Nasder timu ambayo ilikuwa ikifanya kazi na Barakah huenda watu wameliona hilo na kuanza kuongea yao,” alisema Lolly Pop.


