×

Shoga, mbuzi yake kamba mnyororo unamuonea

blackcouple-bedsmileJamani shoga wa mie waooo naona kicheko hadi gego la mwisho kama vile huamini, ndiye mimi Nasra binti Kisoda mjukuu wa Chupa. Namba moja hadi kumi ni zangu wengine kachezeni nje,  kumi bora nimeshika miye.

Kuna kitu kimoja jana kilinikera na kunifanya niwarudishe kwenye unyago,  nikiwa nakwenda zangu mjini nilipanda kwenye daladala na kukaa siti ya nyuma, mbele yangu kulikuwa na wanawake wawili.

Ambao walikuwa wakiongea mambo ya ndani bila aibu, ndiyo maana nikajiuliza kama waliochezwa miaka ya nyuma wamesahau mafunzo ya unyagoni itakuwa wewe unayewekwa saa mbili mbele ya watu eti Kicheni pati, hebu nipishe huko.

Hivi kwanza wewe mwanamke, eeh jamani aibu umeiweka wapi kufikia hatua ya kuyasema maneno ya ndani mwako ndani ya daladala bila hata kugongwa na mshipa wa aibu.

Nilimsikia akisema eti alikorofishana na mumewe na kumsubiri kitandani ndipo alipomkomoa kwa kumkalipia alipomgusa na kumwambia eti. “Nikome”

Weee, mwanamke ndivyo mlivyofu-ndishwa unyagoni kumfanyia mumeo kitandani pale mnapokosana. Hivi unajua madhara ya kumnyima mumeo kata ya maji ukw-eni akiwa na kiu kikali?

Kibaya zaidi upumbavu ulioufanya unamweleza rafiki yako, pengine hata hajui ndoa ni nini, majibu yake mepesi. “Shoga tena mkomeshe wanaume wamezidi.”

Hizi ndizo moja ya sababu ya kumfanya mumeo atembee na house girl, pengine kafikisha umri wa kutumwa sokoni akarudi.

Wewe unamnyima raha alizokutolea kwenu akijua unamkomoa, mwanaume hakomolewi shoga, tupo deiwaka kibao tunatafuta kazi hata ya saa chache, telekeza gari deiwaka alikamate kama tajiri atakukumbuka.

Nataka nizungumze kitu kimoja na wewe mwanamke ni kosa kufungua mahakama kitandani, mwenzio anataka wewe ndio unaanza “unajua,” ajue nini mpe haki yake mashtaka baadae. Niliwaeleza, mtu hawezi kupiga mruzi huku anakula karanga.

Kuna siku nitawapa kisa cha mchota maji kisimani huku akilamba asali, unajua nini alichofanya, asali yote iliishia jichoni badala ya mdomoni. Ndio maana nikasema kuchota maji kuna raha kwa nini ukatishe raha za mwenzako.

Unamnyima mumeo haja zake akamalize wapi, akipata nyumba ndogo inayomjali uanze kupiga kelele.

Hebu wanawake tuache akili za punda wa Dobi. Nakwambia hivi siku mumeo kakuudhi na bado kaja na kata yake kuchota maji kisimani, jua huyo hana ujanja kwako. Utamkomoa kivipi?

Siku hiyo shost jitume ujuavyo mfanyie manjonjo ya kila aina, wakati akitoa sifa kwa uendeshaji wako mzuri wa mashua baada ya safari ndefu, hapo ndipo mpe kilicho moyoni mwako.

Lazima atajua kweli unamthamini pamoja na maudhi yote bado umempa penzi shatashata, lazima atajirudi, mwanaume kwa mwanamke sawa na mbuzi na kamba. Hawezi kwenda mbali ukimfunga mnyororo unamuonea, yangu yameisha tukutane wiki ijayo. Ni mimi anti Nasra Shangingi Mstaafu.

Leave a Comment