×

Wasomaji Wakimbilia kuponi Lala Salama ‘Shinda Nyumba’

????????????????????????????????????
Shadrack Gideon mkazi wa Mkuranga (kulia) akijaza kuponi kushiriki droo kubwa ya Shinda Nyumba.

Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda (kushoto),  akimwelekeza msomaji wa Uwazi, Musa Msumi, namna ya kujaza kuponi.

 

????????????????????????????????????

Mkanda (kulia) akimsaidia msomaji wa gazeti la Uwazi kujaza kuponi.

????????????????????????????????????

Msomaji wa Uwazi, Selemani Abdallah (katikati)  akionyeshwa ukurasa wenye kuponi na Mkanda.

????????????????????????????????????

Mkanda (kulia) akimsaidia msomaji wa gazeti la Uwazi kujaza kuponi.

NA DENIS MTIMA/GPL

WAKATI droo kubwa ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba inafanyika kesho, jana,  Jumanne, wasomaji wa gazeti la Uwazi walijitokeza kwa wingi eneo la Mkuranga-Pwani kununua gazeti hilo baada ya gari la matangazo kutua eneo hilo ambapo wasomaji walilinunua kwa wingi na kujaza kuponi kushiriki shindano hilo.

Bahati nasibu hiyo inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa Magazeti ya Championi, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.

Akizungumza na wakazi wa eneo hilo, Ofisa Masoko wa Global Publishers,Yohana Mkanda, alisema kuwa siku zimeisha hivyo wachangamkie fursa hiyo kwani mshindi anaweza kutoka miongoni mwao.

Katika uhamasishaji huo, Yohana Mkanda alirudia wito wake wa kila mara kwamba: “Siku zimeisha hivyo nunueni magazeti ya Global na mjaze kuponi ili kujiongezea nafasi ya kushinda nyumba kwani unaweza kuwa wewe au yule na kugeuka baba au mama mwenye nyumba! Hivyo, fursa ndiyo hii, bahati humjia mtu yeyote, kwa hiyo nunua Magazeti Pendwa yaliyojaa bahati ya kila namna kila wakati. Kazi kwako, nyumba ndiyo hiyoo…!!!”

Katika droo hiyo ya Shinda Nyumba inayosubiriwa kwa hamu na wasomaji wa magazeti hayo, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda,  ambapo itachezeshewa katika Viwanja vya Zakhem-Mbagala jijini Dar.

 

Leave a Comment