Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesimamishwa kuhudhuria vikao 10 vya Bunge la 11 baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la kuwaonyesha wabunge kidole cha kati wakati akitoka katika ukumbi wa Bunge.

Akisoma taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyosikiliza na kuchunguza kesi hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika amesema wamemkuta na hatia Sugu baada ya kumuoji na kuangalia picha za video pamoja na ushahidi uliotolewa na baadhi ya wabunge walioona tukio hilo.
Bunge limelidhia Mbilinyi kupewa adhabu hiyo iliyopendekezwa na kamati.
