×

Country Boy akunwa na uwezo wa Wizzy Rapper

COUNTRYBOY1Stori: MWANDISHI WETU

RAPA mkali katika Muziki wa Kizazi Kipya, Country Boy, amekunwa na uwezo wa chipukizi Ibrahim Kidugu maarufu kama Wizzy Rapper, aliyeibuka na kibao chake kipya cha Kote Nickike.

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Country Boy alisema Wizzy ni kijana anayekuja vizuri na hatashangaa kama muda mchache ujao, atakamata nafasi ya kuwa mmoja wa marapa bora kabisa katika Tanzania.

“Ukisikiliza hii ngoma yake mpya ndivyo unavyomuona kama mtu anayebadilika kwa ubora ni tofauti na ile ya Nami Nimo aliyomshirikisha Becka Tittle au niliyofanya naye ile ya We on Fire, kwa kweli ninamtabiria makubwa sana huyu mshkaji, kifupi anajua,” alisema.

 

Leave a Comment