×

Kadjanito ajiingiza kwenye filamu

KADJA NITO (5)BONIPHACE NGUMIJE

STAA wa Bongo Fleva ambaye ni zao kutoka jumba la kuibua vipaji (THT), Khadija Said ‘Kadjanito’ ameamua kujiingiza rasmi kwenye filamu.

Akizungumza na mtandao wa Global Publishers, Kadjanito anaye-tamba na Ngoma ya One More Night alisema kuwa kuigiza ni kipaji alichokuwa nacho tangu zamani na kwamba ndoto yake ilikuwa kwanza kuanzia kwenye muziki.

“Napenda sana kuigiza haimaanishi kwamba muziki nimeacha, noo! Siwezi, kwa sasa nimeona tu napo kwenye filamu nina uwezo. Ndiyo kwanza nimetoka kambini kushuti filamu mpya inakuja (jina limehifadhiwa) na mashabiki wakae mkao wa kuniona kwenye filamu nyingi za Kibongo (Bongo Muvi),” alisema Kadjanito.

Leave a Comment