×

Bamboo, Prezzo kufanya ‘media tour’ Bongo

Bamboo_DuecesSimon Kimani ‘Bamboo’

Stori: Boniphace Ngumije

WAKONGWE kwenye gemu la Hip Hop Bongo, Simon Kimani ‘Bamboo’ na Jackson Makini ‘Prezzo’ wanatarajia hivi karibuni kufanya media tour Bongo ili kuupushi wimbo wao mpya uitwao Za Ovyo ambao wameuachia hivi karibuni.

PREZZO5Jackson Makini ‘Prezzo’

Akichonga na mtandao huu dairekti kutoka ‘code’ namba 254, Kenya, Bamboo aliongeza kuwa sababu ya kuja Bongo kwa ajili ya ziara hiyo ni kwamba, kunawashabiki wengi wanafuatilia kazi zao ambao ni muhimu kuwafuata.

“Tunatarajia kuja Bongo hivi karibuni kwa ajili ya media tour na Prezzo, mashabiki zetu huko wakae tu tayari kwa sababu sapoti yao ni jambo la muhimu sana kwetu,” alisema Bamboo.

Leave a Comment