MSANII wa Bongo Fleva, Baby Madaha haishi vituko na safari hii, amekuja na mpya kwamba eti mchumba wake, raia wa Dubai amemzuia kufanya muziki kwa muda ili asimamie biashara na mambo mengine ya kifamilia.
“Nimepumzishwa kwa muda na mchumba wangu kwa ajili ya kuangalia biashara zetu na mambo mengine ya familia, kwa hiyo namsikiliza kipenzi changu,” alisema Madaha.
Baby Madaha, msanii ambaye pia hufanya filamu, amekuwa mtu wa vitimbwi vingi, kama hivi karibuni alipodai kuwa hawezi kushiriki mapenzi na kapuku na vilevile aliwahi kudai, hana mpango kabisa wa kupata mtoto kwa sasa kwa vile bado anakula maisha.
