MSANII wa Muziki wa Injili anayetamba na Wimbo wa Ipo Siku, Goodluck Gozbert amesema lengo lake kwa sasa ni kufanya kazi na mwimbaji kutoka nje ya nchi, kwani anahitaji kutoka kimataifa zaidi.
Akizungumza na Mtandao wa Global, Goodluck alisema kwa hapa nyumbani hajamuona mwimbaji wa kufanya naye kolabo, ndiyo maana kwa sasa yupo ma mazungumzo na wasanii wa nje ya Bongo.
“Sijawahi na sifikirii kufanya kolabo na staa wa Injili wa hapa Bongo, bali nina mpango wa kwenda kimataifa zaidi na sasa niko kwenye mazungumzo na wasanii tofauti japokuwa siwezi kuwataja kwa sasa, muda ukifika nitawajuza mashabiki wangu,” alisema Goodluck.
