×

Hatimaye Oscar Pistorius ahukumiwa kwenda jela

PISTORIOUS-3.jpgOscar Pistorius

Mwanariadha mlemavu wa miguu wa Afrika Kusini aliyejinyakulia mataji kibao ya Olympic, Oscar Pistorius leo amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela  kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp.

PISTORIOUS-2.jpg

Pistorius mwenye umri wa miaka 29 alionekana mwenye huzuni jspo akijikaza wakati hukumu hiyo ikisomwa dhidi yake huku familia yake ikishindwa kuzungumzia chochote kuhusiana na tukio hilo.

oscar-pistorius-800.jpg

Baadhi watu waliofika kusikiliza hukumu ya kesi hiyo wamedai kuwa, hukumu iliyosomwa Jaji Thokozile Masipa wa mahakama hiyo muda mfupi uliopita kuhusu tukio la Pistorius kumuua mpenzi wake ni ndogo ikilinganishwa na kosa alilotenda huku wakieleza kuwa alimuuwa Reeva kwa makusudi wala sio kwa bahati mbaya. Awali Pistorius alikuwa anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela baada ya vita ya kisheria iliyochukua takriban miaka mitatu.

PISTORIOUS-4.jpgWazazi wamarehemu Reeva Steenkamp.

Mwanariadha huyo Oscar Pistorius tayari ameshatumikia kifungo cha takribani miezi tisa jela katika kosa la awali wakati alipopatikana na hatia ya kuua bila kukusudia mwaka 2013.

jajiJaji Thokozile Masipa.

Jaji Thokozile Masipa ameieleza mahakama hiyo kuwa, endapo Oscar Pistorius atamaliza nusu ya kifungo chake bila matatizo, basi mahakama hiyo inaweza kumbadilishia adhabu kwa kumpa kifungo cha nje kwa muda utakaokuwa umesalia kukamilisha adhabu.

Mahakama pia ilitoa ruksa kwa mawakili wa Oscar Pistorius kukata rufaa japo walikataa na kususia kufanya hivyo kwa ajili ya mteja wao.

Leave a Comment