×

Aunt awehuka barabarani, asababisha foleni!

aunty-ezekiel34Stori: IMELDA MTEMA, RISASI JUMAMOSI

DAR ES SALAAM: Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amewashangaza watu baada ya juzikati kushuka kwenye gari yake aina ya Toyota Alphard na kuanza kucheza huku akilizunguka gari hilo.

Tukio hilo la kushangaza lilitokea Sinza Mori jijini Dar majira ya saa mbili usiku ambapo inadaiwa chanzo ni simu yake aina ya S7 Edge kugoma kuonyesha mtandao na alipojaribu kupeleka kwa fundi akaambiwa itakuwa imezimwa na TCRA.

“Awali Aunt alichanganyikiwa sana baada ya simu yake kutoonyesha mtandao na alipopeleka kwa fundi aliambiwa imezimwa na TCRA,” kilidai chanzo.

Mpashaji wetu huyo aliendelea kufunguka kuwa baada ya kuambiwa hivyo staa huyo akakosa amani kabisa huku akifikiria ni jinsi gani atanunua simu nyingine.

Chanzo chetu hicho kinazidi kufunguka kuwa, akiwa njiani ndani ya gari lake akitoka kwenye mishe zake alipata wazo la kutoa laini iliyokuwa ndani ya simu yake na kuweka nyingine ambapo alipojaribu tu mtandao ukasoma, kitu kilichompa furaha ya ajabu na kiwewe.

“Furaha aliyoipata baada ya kugundua kuwa simu yake haijazimwa ila tatizo ni laini, ndiyo ilimuwehusha, alianza kurukaruka, akasimamisha gari barabarani akashuka na kusababisha foleni,” kilizidi kunena chanzo hicho.

Baada ya kupata udaku huo gazeti hili lilimpigia simu Aunt, alipopatikana alisema: “Jamani hata kama ni wewe imekutokea simu yako ya milioni na kitu imezima ghafla lazima akili isiwe vizuri, kilichotokea nilipata furaha ya ajabu kwa kweli.”

Leave a Comment