
NA LEONARD MSIGWA MTANDAO/GPL
Wapiganaji tishio wa kikundi hatari cha kigaidi cha ISIS kimewaua kwa kuwakata vichwa wachezaji wanne Osama Abu Kuwait, Ihsan Al Shuwaikh, Nehad Al Hussen na Ahmed Ahawakh waliokuwa wakiichezea timu maarufu ya Al-shabab ya nchini Syria.
Wachezaji wanne maarufu nchini Syria wakiwa wameuawa na ISIS.
Walitekeleza mauaji hayo kwa kuwatuhumu wachezaji hao kulipeleleza kundi la kigaidi la Kurdish, katika mauaji hayo pia aliuliwa raia mwingine ambaye jina lake halikufahamika. Katika picha zilizosambaa mtandaoni zinaonesha watoto wadogo wakitumika kukagua maiti hizo kama njia ya kuwatia hofu zaidi watoto wadogo kushirikiana na serikali nchini Syria.
ISIS walipiga marufuku michezo yote kwenye mji wa Raqqa yaliyotokea mauaji hayo miaka miwili iliyopita. Mwaka mmoja uliopita wapiganaji wa ISIS waliwaua vijana wa kiume 13 kwa kuangalia mechi ya mpira wa miguu, kombe la mataifa ya Asia kati ya Iraq na Jordan.
Vijana hao wa kiume walikamatwa wakiangalia mechi kwenye televisheni jijini Mosul, Iraq mji unaoshikiliwa na ISIS. Waliwekwa katika mzunguko wa duara na kisha kumiminiwa risasi hadharani. Imeripotiwa mauaji yamekuwa yakifanyika kwa siri nchini Iraq na Syria kwa watu wote wanaopingana na ISIS.

huyo ni shetani mpinga kristo anaekuja kwa sura ya binadam(ISIS)