Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Dkt. Adelhelm Meru akiweka pakiti za Whitedent ndani ya moja ya magari yatakayoshindaniwa.
…Meru akijaza pakiti za Whitedent ndani ya Suzuki Alto 10.
Dkt. Adelhelm Meru akishiriki kujaza kuponi ya bahati nasibu hiyo. Anayemshuhudia Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Bala Balasubramaniam.
Dkt. Adelhelm Meru Bala na Mkurugenzi Mkuu wa Chemi & Cotex Ltd, Bala Subramaniam wakiteta jambo katika hafla hiyo.
Warembo wa Kampuni ya Chemi & Cotex Ltd wakisimamakwenye magari yatakayoshindaniwa.
Viongozi hao wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Mer (katikati).
Keki maalum iliyokuwa imeandaliwa.
KAMPUNI ya bidhaa za afya ya mdomo Whitedent, leo imezindua promosheni yake ya miezi mitatu ya wananchi kujishindia magari 25 ya aina ya suzuki Alto K10
Uzinduzi huo umefanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar ikiwa ni siku yake ya kusherehekea kutimiza miaka 25 ya Kampuni ya Chemi& Cotex Industries Ltd tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza katika hafla hiyo, Ofisa Mkuu Chemi&Cotex, Raja Swaminathan alisema kuwa, wanatoa nafasi kwa maelfu ya wananchi kushiriki shindano hilo kwa kukisia idadi ya pakiti za Whitedent zilizomo ndani ya moja ya magari hayo ya Suzuki litakalokuwa linazunguka nchi nzima wakati wa promosheni.
Alisema mteja atakachotakiwa kufanya ni kujaza fomu ya ushiriki katika kipindi hicho cha promosheni na kukisia jibu sahihi ili aweze kuingia ktika droo kubwa ya kujishindia moja ya magari hayo ambapo mwisho wa promosheni hiyo ni Oktoba mwaka huu.
“Katika kusherehekea miaka 25 ya bidhaa hii tumetaka kuwashirikisha wananchi wote katika mafanikio yetu.Tunatoa magari haya ambayo ni mapya kabisa yakiwa yamejaa mafuta kwenye tenki lake na yakiwa yamelipia ushuru na bima kwa muda wa mwaka mzima na wala hakutakuwa na kiingilio chochote wala kiasi cha pesa ili mwananchi aweze kushiriki zaidi ya hapo watu wote wanaweza kushiriki mara nyingi wawezavyo,” alisema Swaminathan.
Aidha alisema promosheni hiyo itakuwa chini ya uangalizi mkubwa wa Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania ambapo itashirikisha mikoa yote na Visiwani Zanzibar.
“Tungependa kila mtu awe na nafasi ya kushiriki katika shindano hili kwani itapita mijini na vijijini kote ili kila mwananchi aweze kuibuka na magari hayo,” aliongeza Swaminathan.
Swaminathan aliendelea kutoa ufafanuzi kuwa inakadiriliwa zaidi ya wana Afrika Mashariki milioni 14 huanza siku yao kwa kupiga mswaki kwa kutumia Whitedent ambapo alieleza kwa mujibu wa ukaguzi wa Nielsen wa mwaka 2012 ulionyesha Whitedent asilimia 79 ya soko nchini na hupatikana katika maduka makubwa na vibanda vidogo.
“Mafanikio makubwa ya Whitedent yanaonyesha kuwa uwezo wa viwanda nchini kwetu ni mkubwa na tuna nafasi kubwa ya kukua na kutengeneza bidhaa bora kwa Watanzania kwa bei nafuu na pia kuweza kuuza ulimwenguni kote. Tunajivunia kuwa katika viongozi wa mafanikio haya,” alisema Swaminathan.
Naye Mgeni rasmi wa hafla hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru aliupongeza uongozi mzima wa Kiwanda cha Chemi & Cotex Industries Ltd kwa kuzalisha bidhaa yake iliyo bora na inayopendwa na Watanzania huku akisema serikali itaendelea kuwasaidia kuendeleza uchumi wa viwanda na kuwaasa wananchi kupenda bidhaa inayozalishwa hapa nchini.
Shindano hilo limezinduliwa leo katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Musoma ambapo pia promosheni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa Julai 14 mwaka huu katika mikoa ya Morogoro,Tabora, Kilimanjaro, Mtwara, Iringa, Kigoma na Shinyanga.
NA DENIS MTIMA/GPL

