×

Polisi Yakamata Gamba la Kasa, Meno ya Tembo 666

Diwani Athumani (1)

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Diwani Athuman, akisoma taarifa kuhusu tukio hilo.

Diwani Athumani (2)
…Akiendelea kuwasiliana na wanahabari (hawapo pichani).

wanahabari (1)
Wanahabari wakichukua tukio hilo.

JESHI la polisi nchini kwa kushirikiana na ofisi za polisi wa kimataifa (Interpol) Kanda ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Regional Police Chiefs Cooperation Organization) imekamata gamba moja la kasa mkoani Ruvuma na vipande vya meno ya tembo 666 vyenye kilo 1279.19 vikiwa na thamani zaidi ya Sh. Bilioni Nne.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Diwani Athuman, alisema kuwa vipande hivyo vya meno ya tembo vimehusisha watu tisa kati yao ni raia wa Uganda na mwingine raia wa Guinea.

Amesema kuwa katika operesheni inayoitwa Usalama III wamekamata vitu mbalimbali kutokana na taarifa za kiintelijensia zilizokusanywa wakati wa matayarisho ya operesheni hiyo ambapo walikamata mitambo 18 ya kutengenezea pombe ya gongo na lita 960 za gongo zilikamatwa.

Athuman alisema katika operesheni hiyo wamekamata watuhumiwa 265 ambapo baada ya uchunguzi wataobainika kuhusika na vitendo vya kihalifu watafikishwa mahakamani.

Alitoa rai kwa wanunuzi wa magari nje ya nchi kuwasiliana na ofisi za Interpol za ndani au nje ya nchi kuhusu magari yanakotoka kwa uchunguzi ili kuwafanya wanunuzi kununua magari halali na kuondoa usumbufu wa kukamatwa katika operesheni kama hizo.

Aliongeza kuwa jeshi la polisi halitakubali kuona kundi la watu wachache linatishia usalama wa maisha ya raia wema na mali zao hivyo wataobainika kufanya hivyo litawachukuliwa hatua za kisheria bila kusita.
Oparesheni hiyo ilizishirikisha idara na taasisi za kiserikali ikiwemo: Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Ushuru wa Forodha (TRA).

NA DENIS MTIMA/GPL

 

Leave a Comment