Lagos, Nigeria
STAA wa muziki nchini Nigeria, Iyanya amekumbata na kashfa ya kudaiwa ‘kufulia’ kiasi hadi kufikia kiasi cha kutokuwa na pesa ya kulipia bili yake hotelini wakati akiwa kwenye tour ya shoo yake nchini Marekani hivi karibuni.
Kashfa hizo zimetolewa hivi karibuni na mwandaaji wa matamasha maarufu nchini humo, Promota Don De Moe baada ya kuufahamisha ulimwengu kupitia mtandao wa Instagram kuwa staa huyo hana chochote kwa sasa kwani hata bili anayodaiwa na hoteli ya Hilton ameshindwa kulipa, jambo ambalo limemdharirisha Iyanya.
Don De Moe alisema “Iyanya, nakuomba ulipe bili yako unayodaiwa kwenye hoteli ya Hilton,” Moe aliongeza tena kuwa, “Hujalipa bili yako tangu Jumatatu, Julai 4th na nimechoka ‘kukubeba’ (kukusaidia).”
Baadaye Iyanya naye akajibu “Watu wenye chuki chuki (maadui) wanataka kumfanya mtu mwema aonekane mbaya.”
Maneno hayo yaliwadhihirishia mashabiki wa Iyanya sata wa “Kukere“ kuwa hajafirisika kiasi cha kushindw akulipa bili ila yawezekana kuna kutofautiana kati yake na Don De Moe.
Tangu atangaze kuihama lebo ya MMMG (Made Men Music Group) na kuyanzishga lebo yake mwenyewe, mambo mengi yamekuwa yakiandikwa kuhusu Iyanya aliyebamba na wimbo wa “Oreo“ huku akizungumzwa vibaya hususan watu aliyokuwa akifanaya nao kazi kwenye lebo hiyo.
MMMG pia ina wasanii kama Tekno, Selebobo, Mr Chibbz, na Tonye Garrick.

