

Andria, Italia
Treni mbili zimegongana kusini mwa nchi ya Italia na kuua watu 12 eneo la tukio na wengi wao kujeruhiwa.
Treni hizo kila moja ikiwa na mabehewa manne ziligongana kwenye mji wa Andria uliopo kwenye Jimbo la Puglia.
Waziri Mkuu wa Italia, Renzi amesema, “huu ni wakati wa majonzi ambapo sote kwa pamoja tunapaswa kuungana kuwafariji wafiwa na kuwatibu majeruhi.”
Treni zilizogongana moja ilikuwa ikitoka Andria na nyingine Corato.