HABARI njema! Kwa mara ya kwanza, staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha amejikuta akitoa meno yote nje, baada ya kuvishwa pete ya uchumba na mwanaume wake mwenye asili ya Kiarabu aishiye Dubai.
Akiteta na Risasi Vibes, Baby alisema anamshukuru Mungu kwa hatua hiyo kwani alikuwa akiitamani kwa muda mrefu na kwamba ndoa itakuja ‘soon’ japo itakuwa ya kimyakimya.
“Nimefurahi sana na ndoa inakuja soon, sikuwahi kuvishwa pete na mwanaume yeyote hapo awali kama walivyo wasanii wengine, namuomba Mungu anisaidie ili niweze kufanikisha suala hilo la ndoa,” alisema Baby Madaha.
