×

Mafua kwa maji ya kitunguu chekundu, asali

asaliMwezi huu una baridi sana na watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na mafua na wengine wanajikuta wana aleji  hata za mwili kuwashwa na ngozi kuonekana haipo sawa.

Ili kuwa sawa, tumia maji ya kitunguu chekundu kwa kipindi hiki.

Kitunguu chekundu kina kemikali yenye mchanganyiko wa Quercetin, ambayo inasaidia kuweka sawa mwili pale unapokutana na fatiki.

Quercetin pekee ni kemikali inayosaidia kufungua matundu yaliyoziba ambayo yanasaidia hewa kupita hivyo kwa kutumia kitunguu, husaidia sana kuondoa magonjwa.

Mahitaji

Maji vikombe 4

Kitunguu chekundu-1

Asali mbichi

Chukua kitunguu, kikatekate vipande, weka kwenye maji kisha changanya na asali vijiko viwili vikubwa. Baada ya kuchanganya mchanganyiko huo, acha kwa muda wa saa nne mpaka 12 kabla ya kunywa.

Baada ya hapo kunywa kwa siku mara mbili, kipimo unaweza kujipimia mwenyewe, pia kama una friji unaweza kuiweka kwa siku nne wakati unakunywa ikishazidi siku hizo usitumie kabisa.

Leave a Comment