×

Bella kufanya sapraizi Dodoma

BELLAMwandishi wetu

BAADA ya kufanya bonge la shoo wikiendi iliyopita lililojulikana kama Black Tie ndani ya Dar, King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kufanya sapraizi katika shoo nyingine kubwa itakayofanyika Julai 22, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Royal Village, Dodoma.

Akizungumza na Amani mratibu wa shoo hiyo, Renatus Gregory alisema kuwa usiku huo Bella atapiga nyimbo zake zote kali tangu ameingia rasmi Bongo.

“Kwa mara ya kwanza, Bella atatimiza miaka 10 pia ndani ya Dodoma ambapo atapiga nyimbo zake zote kuanzia, Yako Wapi Mapenzi, Safari Sio Kifo, Nashindwa, Amerudi, Nani Kama Mama na nyingine kibao,” alisema Renatus.

Usiku huo kiingilio kitakuwa shilingi 30,000 kwa VIP na kawaida shilingi 10,000.

Leave a Comment