×

Digital kutoka na Chokoraa

chokoraa-copyMSANII aneyepanda kwa kasi kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, anayefahamika zaidi kwa jina la Digital amefunguka kuwa moja ya wasanii anaohitaji kufanya nao kazi kwa sasa ni mkali aliyekuwa akiunda Kundi la Mapacha Watatu, Khalid Chokoraa.

Akistorisha na Showbiz Xtra, Digital ambaye ni mmoja wa wasanii wanaounda Bendi ya La Musica Vijana Classic alisema uongozi wake uko katika harakati za kumtafuta Chokoraa na akipatikana atafanya naye kazi.

“Ninamzimia sana Khalid Chokoraa ni mwalimu na ni msanii ambaye ninamuota kila siku kufanya naye kazi. Hilo nimelifikisha mbele ya uongozi wangu na wanalifanyia kazi,” aliweka kituo Digital.

Leave a Comment