×

TRA, NMB Hukusanya Kodi Sh. Bil 19.8 kwa Mwezi

????????????????????????????????????Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili akizungumza na waandishi kuhusu  mfumo mpya wa ulipaji kodi unaofanywa na TRA na NMB. Kulia ni Meneja wa Hesabu za Mapato wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ramadhan Sengati na Mkuu wa Kitengo cha Malipo wa Benki ya NMB, Michael Mungure.

????????????????????????????????????Baadhi ya wanahabari wakisikiliza mkutano huo.

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????Maafisa wa NMB na TRA wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Na mwandishi wetu/GPL

KUFUATIA maboresho ya mfumo wa ulipaji kodi kurahisishwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ kushirikiana na Benki ya NMB hukusanya Sh. Bil. 19.8 kwa mwezi kama malipo ya kodi ya wateja wanaotumia benki hiyo.

Awali ya mfumo na urahisishwaji wa ulipaji huo, TRA na Benki ya NMB walikuwa wakikusanya mapato ya kodi ya Sh. Bilioni nane hadi 14 kwa mwezi.

Alisema hatua ya kuboreshwa kwa mfumo huo wa Tehama umechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa mawasiliano imara kati ya TRA na NMB wakati mteja anapotaka kufanya malipo ya kodi.

Akizungumza na wanahabari leo Makao Makuu ya Benki ya NMB yaliyopo Posta jijini Dar,  Meneja wa Hesabu za Kodi TRA, Ramadhan Sengati alisema: “Kwa sasa mfumo huu huo mpya na rahisi unatuwezesha kujua moja kwa moja malipo yanayofanywa na wateja wa NMB hivyo hakuna aina yoyote ya udanganyifu kama ilivyokuwa awali. Taifa lolote  lile  haliwezi kuendelea kama wananchi wake hawako tayari kulipa kodi kwa hiari.”

Leave a Comment