KING of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kupiga shoo ya live kwa kutumia vyombo kwa mara ya kwanza Julai 22, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Royal Village, Dodoma.
Akizungumza na Burudani Mwanzo Mwisho, mratibu wa shoo hiyo, Renatus Gregory alisema kuwa usiku huo Bella atakuwa akitimiza miaka 10 tangu aingie kwenye muziki nchini.
“Kwa mara ya kwanza Bella atatimiza miaka 10 pia ndani ya Dodoma ambapo ataimba nyimbo zake zote na mashabiki wake kuanzia, Yako Wapi Mapenzi, Safari Sio Kifo, Nashindwa, Amerudi, Nani Kama Mama na nyingine kibao,” alisema Renatus.
Usiku huo kiingilio kitakuwa shilingi 30,000 kwa VIP na kawaida shilingi 10,000.
