×

50 Cent: Kanye west, Donald Trump ndiyo walewale tu

_kim-kardashian-kanye-west-NEW YORK, Marekani

RAPA Curtis Jackson a.k.a 50 Cent akiwa katika mahojiano aliyofanyiwa hivi karibuni, amegusia kuhusiana na hatua ya mume wa Kim Kardashian, Kanye West kutaka kuwania urais wa Marekani 2020.

50Centfiledforbankruptcyafterwasorderedtopay5milliontoLastoniaLevistonincourtaftershesaidhepostedasextapeofheronline.jpg 50 Cent

Katika mahojiano na Conan O’Brien, 50 alipoulizwa kuhusiana na uamuzi huo wa Kanye alijibu huku akionekana kukejeli: “Nimependa wazo lake la kuwania urais, lakini unajua kwamba urais una majukumu mengi, naweza kusema wako sawa au ni kama vile ilivyo kwa Trump (Donald).”

Donald-TrumpDonald Trump

50 alimaanisha kuwa ni ngumu kwa Kanye ambaye ni hasimu wake wa muda mrefu kushinda au kuhimili majukumu ya urais kama vile inavyoonekana kwa Trump anayetajwa kuwa kwenye hatari ya kukosa kura nyingi kwa Wamarekani weusi kutokana na ukorofi wake.

Leave a Comment