Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba (kushoto) aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/16 akisalimiana na Afisa Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary (kulia)wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombela.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba (kushoto) aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/16 akiteta jambo na Afisa Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary (katikati) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombela.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/16 akiongea wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/16 akimkabidhi tuzo mchezaji wa yanga Abdul Juma,aliyeibuka mchezaji bora wa mwaka wa ligi. Hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/16 (kushoto) akimshuhudia Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Domician Mkama (kulia) akimpongeza mchezaji wa yanga Abdul Juma,aliyeibuka mchezaji bora wa mwaka wa ligi. Hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Simba,Mohamed Hussein Shabalala (kushoto) akipokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 4/- toka kwa Afisa Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary kwa kuibuka mshindi wa mchezaji bora chipukizi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016 wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi hiyo.
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya Dar es Salaam,Domician Mkama (kushoto) akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi 80.7 mwakilishi wa timu ya Yanga kwa kuibuka mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.Wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/16 (kushoto) akimshuhudia mchezaji wa Yanga Abdul Juma, akiwaonesha waandishi wa habariri tuzo yake aliyoshinda ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu.Wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/16 (watano kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa TFF na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania pamoja na washindi wa tuzo mbalimbali mara baada ya hafla hiyo kuisha iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
1. Mchezaji Bora: Juma Abdul – YANGA
2. Golikipa Bora: Aishi Manula – Azam FC
3. Kocha Bora: Hans Van Pluijm – YANGA
4. Mchezaji Bora Chipukizi: Mohammed Hussein -Simba
5. Mchezaji Bora wa Kigeni: Thabani Kamusoko – YANGA
6. Mfungaji Bora: Amiss Tambwe – YANGA
7. Goli bora la Msimu lilifungwa na Ibrahim Ajib
8. Timu yenye nidhamu: Mtibwa Sugar
9. Mwamuzi Bora: Ngole Mwangole – MBEYA
10. Zawadi za Washindi
i) Mabingwa – YANGA Sh. Milioni 81.3
ii) Washindi 2 – AZAM Sh. Milioni 40.6
iii) Washindi 3 – SIMBA Sh. Milioni 29
iv) Washindi 4 – TZ PRISONS Sh. Miloni 23.2








