×

Mke wa Trump Aigiza Hotuba ya Michelle Obama

wife wa trump

Mke wa Donald Trump, Melania Trump.

Na Leonard Msigwa/GPL

MKE wa mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump, aitwaye Melania Trump, usiku wa kuamkia leo ametia aibu baada ya hotuba yake ya kwanza aliyoitoa jana kwenye kongamano la chama cha Republican kubezwa na watu wengi nchini Marekani.

Watu wengi wanasema amenakili mistari mingi kutoka kwenye hotuba ya kwanza ya Michelle Obama aliyoitoa mwaka 2008 wakati mumewe Barack Obama akiomba ridhaa ya mkutano mkuu kumpitisha kuwa mgombea urais kupitia chama cha Democratic.

mary-pat-christie-donald-trump

Miongoni mwa maneno aliyonakili mwanamke huyo ni yale yaliyozungumzia umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii uliokuwa na maneno ya Michelle Obama ya “Work hard for what you want in life” yaani kitafute kwa juhudi kile unachokitaka maishani mwako.

Pia alinakili msemo unaohusu dhamira anayotamka mtu kama ahadi usemao kwamba “Your word is your bond.”

Maneno mengine aliyonakili ni yale yanayozungumzia umuhimu wa kuwalinda watoto na kuwapa mahitaji muhimu ambayo ni “We want our children in this nation… to know that the limits of your achievements is the reach of your dreams and your willingness to work for them.

Republican-National-Convention-Cleveland-USA-18-Jul-2016

Donald Trump na Melania Trump.

Mitandao mingi nchini Marekani hususani ile ya kijamii imekuwa ikikosoa vibaya hotuba hiyo kwa kile kinachoonekana kuwa hakuna jambo jipya zaidi ya kunakili maneno ya Michelle Obama.

 

 

Leave a Comment