KLABU ya Machester United (Mashatani Wekundu) inayonolewa na kocha Mreno Jose Mourhino imefikia makubaliano ya awali ya kumsajili kiungo hatari wa timu ya Juventus raia wa Ufaransa, Paul Pogba katika usajili utakaogharimu paundi za Uingereza milioni 87 sawa na Euro milioni 104.
Mawakala wa Manchester United wanategemea kukutana na viongozi wa Juventus pamoja na wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aitwaye Mino Raiola leo mchana kwa saa za Italia.
Pogba tayari amefanya makubaliano ya awali na klabu ya Manchester United ambapo atapokea mshahara £10.92m (13m Euros) kwa mwaka na ndani ya saa 24 kuna uhakika wa kutua klabuni hapo.
Uamisho huo umepongezwa na gwiji wa zamani wa timu ya Arsenal na Barcelona Thierry Henry ambaye amesema uhamisho huo utaifaidisha timu ya Manchester United na kufanya ligi hiyo izidi kuwa na mvuto duniani.
“We all know about the quality, how good he is on the ball, he’s an all-round player but he understood his role at the tournament (Euro 2016). “Hopefully he can come back to the Premier League – it would be great for us and for whoever got him but he’s still a Juve player and they’re not going to let him go (easily).” Alisisitiza Thierry Henry.
