Grace Malikita
Na Gabriel Ng’osha
WIKI iliyopita mrembo Grace Malikita alishinda Taji la Miss Tabata mwaka 2016 kwa kuwapiga chini warembo 15 wengine, huku nafasi ya pili akishika Nasra Munna na nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Mariam Maabadi.
Shindano hilo lililofanyika Ukumbi wa Dar West Park uliopo Tabata jijini Dar, warembo wengine waliofanikiwa kuingia Tano Bora ni Sabrina Kipuga, Jackline Evarest na Neema Makwaia.
Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers likisindikizwa na burudani ya muziki wa dansi kutoka kwa bendi kongwe ya Tanzania African Stars ‘Twanga Pepeta’ pamoja na wasanii wengine.