Daud Mwangosi.
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa leo imemtia hatiani, Pacificius Cleophace Simon ambaye ni mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa, Daud Mwangosi kwa kuua bila kukusudia.
Mahakama imesema itatoa hukumu ya kesi hiyo keshokutwa Julai 27, mwaka huu.
Pacificius anatuhumiwa kumuua Mwangosi katika tukio lilitokea katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi Mkoani Iringa Septemba 2, 2012.
