×

Babu Tale Mbaroni kwa Kutomlipa Sheikh Mbonde Mil 25

babu-tale

Hamis Tale Tale ‘Babu Tale’.

Meneja wa staa wa Bongo Flavour Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale ‘Babu Tale’ amefikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutoa sababu za kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya shilingi milioni 25 kwa makosa ya kuvunja sheria ya hakimiliki.

Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Sheikh Mbonde kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya sheikh huyo jambo ambalo ni kinyume na hakimiliki.

Leave a Comment