Ofisa Usambazaji wa Global, Jimmy Haroub (kulia) akimuuzia gazeti la Uwazi, Ally Mafita mkazi wa Mabwepande.
Cleophace Mgeta (katikati) mkazi wa Mabwepande akiuziwa Uwazi na Jimmy Haroub (kushoto).
Msomaji wa Uwazi aitwaye, Ibrahim Gideon akilisoma Uwazi baada ya kulinunua.
Wadau wa Uwazi wa eno la kituo cha daladala cha Mabwepande wakisoma gazeti lao.
Mwanadada aitwaye, Rehema Shomari akisoma Uwazi.
Mdau wa Uwazi, Abrahaman Chelewa (kulia) akisoma Uwazi.
Billy Mhando (mwenye kofia) akisoma Uwazi. Anayemshuhudia ni Jimmy Haroub.
Godlove Mushi (kulia) akipozi na Haroub baada ya kununua gazeti la Uwazi.
Jimmy Haroub (kulia) akimshuhudia msomaji wa Uwazi, James Msumba, akisoma gazeti lake.
Musa Shaban (kushoto) akielekezwa na Jimmy Haroub baadhi ya hadithi zilizomo ndani ya gazeti hilo.
GAZETI la Uwazi linalotoka kila siku za Jumanne, leo lilitinga maeneo ya Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar na wasomaji wa gazeti hilo kuonekana kulichangamkia kulinunua.
Miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa ni Mabwepande na maeneo ya Mpigi-Magohe ambayo wasomaji wa Uwazi walionekana kulinunua kwa wingi.
Ofisa Masoko wa kampuni ya Global Publishers inayozalisha gazeti hilo pamoja na Ijumaa Wikienda, Ijumaa, Risasi, Amani na Championi katika eneo la Mabwepande, Yohana Mkanda, alisema anawaomba wasomaji wa magazeti hayo ya Global kuendela kulinunua Uwazi kwa bei ya Sh.500 kwani limesheheni habari nyingi za uchunguzi, hadithi, machombezo na mikasa.
“Magazeti yote ya Global yanauzwa kwa shilingi 500 isipokuwa Ijumaa pekee lenye muonekano mpya ndilo linauzwa shilingi 1,000 (elfu moja). Niwasihi wasomaji wetu waendelee kununua magazeti yetu ili wazidi kuhabarika, kuelimika na kuburudika,” alisema Mkanda.
NA DENIS MTIMA/GPL

