×

Etihad Yazindua Vyumba vya Mapumziko ya Kisasa Uwanja wa Los Angeles

Etihad (1) Etihad (2)

Etihad (5)

Muonekano wa eneo la mapumziko ya kisasa yaliyozinduliwa na Etihad kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Los Angeles, Marekani.

Etihad (3)

Uzinduzi wa Etihad Airways First & Business Class Lounge mjini Los Angeles, Marekani ukifanyika.

Picha zaidi zinapatikana: HAPA 

  • Uzinduzi wa eneo hilo la kisasa ni kuonyesha dhamira yetu kwa Marekani na wateja wetu ukanda wa magharibi.
  •  Eneo lina huduma muhimu, likiwa na hoteli za hadhi ya juu na huduma nzuri ya hoteli.
  •  Vyakula mchanganyiko vilivyoandaliwa na wahudumu wenye uzoefu vinapatikana.
Shirika la Ndege la ETIHAD limezindua rasmi sehemu ya kupumzika kwa daraja la kwanza na kati katika eneo la  Tom Bradley  katika uwanja wa kimataifa wa Los Angels. Ujenzi huo umeendana na ubora na kiwango cha huduma zinazotolewa, ikiwa ni ahadi ya huduma bora kwa wateja wa madaraja ya kwanza na kati wanaotumia ndege ya Etihad ya EY170 Boeing kutoka Marekani Magharibi na ukanda wa pwanai na kitovu cha burudani.

Pamoja na sehemu yenye hadhi ya juu ya kupumzika ya Etihad iliyopo Washngton DC na New York, huduma hii ya kwanza Los Angles(LA) imewekwa ili kuonyesha ukarimu kwa Wamerakani, ni huduma ya kwanza katika ukanda wa  Marekani Magharibi.

Huduma zinazopatikana katika sehemu za mapumziko kwenye viwanja vya ndege vinavyohudumiwa na ndege za Etihad zimewekwa kuendana na utamaduni wa Kiarabu  unaopatikana kwenye utamaduni wa Abu Dhabi.

Makamu wa Rais wa Shirika la Ndege la Etihad, Martin Drew alisema” Ikiwa ndilo shirika linaloongoza kwa huduma za anga ulimwenguni, Etihad imeendelea kuboresha huduma, na kuwa kiongozi kwenye ubunifu wa huduma zake kwa wateja ndani ya ndege na wawapo sehemu ya kupandia ndege.

“Sehemu yetu mpya ya mapumziko kwa wateja wa daraja la kwanza na la pili mjini Los Angles, imedhihirisha dhamira yetu kwa abiria wa ukanda wa marekani ya magharibi na Marekani kwa ujumla, kwa kutoa huduma bora iliyokuwa inatarajiwa na wateja wetu. Hii ni heshima kubwa kuzindua huduma hii.”

etihad (1)

Wahudumu katika eneo hilo.

LAWA (Los Angles World Aiprorts) na washirika wetu wa ndege wamedhamiria kuboresha huduma ndani ya ndege na kwa wageni wetu  wanaosubiri kusafiri  ili wapate kile kinachostahili.” Alisema Ofisa Mtendaji wa Los Angels Word Airpot.

Sehemu hiyo ina hoteli yenye ubora pia yamewekwa mazingira ya kuwahudumia watu hata wakiwa wengi. Sehemu mpya ya mapumziko inamwezesha mteja kuwa huru, kuburudika na kufurahia huduma kutoka kwa watoa huduma  wa ndege  za Etihad wenye uzoefu wa kutosha.

Kuna sehemu nzuri yenye kukufanya ujisikie vizuri ikiwa na viti vya kukaa, sehemu ya kupata mlo, bar na eneo la kutazama runinga, sehemu ya kuoga, sehemu ya matumizi ya mtandao ikiwa na soketi za kutumia USB pamoja na chumba cha magazeti na majarida ya ndani na nje ya nchi.

 

Eneo maalumu limetengwa likiwa na huduma zote muhimu

Eneo hilo lililopo pembezoni, linaonekana  kwenye eneo lenye maduka ya kisasa, hivyo sehemu hiyo ya mapumziko ya Etihad kwenye uwanja wa Los Angels imefunguliwa maalaumu kwa ajili ya wateja wa daraja la kwanza na kati wanaotumia ndege aina ya EY170.

etihad (2)

Baadhi ya vyakula vinavyopatikana eneo hilo.

Huduma za Los Angels zimeongeza ubora wa huduma kwa wateja wanazozipata kwenye karibu vituo 15 ikiwamo kile cha Abu Dhabi. Miongoni mwa vituo hivyo ni kile cha Lounge and Spa kinachopatikana Terminal 3; Premium Lounges katika Terminals 1 na 3; Premium Lounge  nchini Marekani), Frankfurt, London, Manchester, Dublin, Paris, Washington D.C., New York JFK, Sydney na Melbourne.

Huduma za ndege za Etihad limekuwa likitoa huduma zake kati ya Los Angeles Na Uwanja wa Kimataifa wa Abu Dhabi tangu Julai Mosi 2014. Vilevile huduma za usafiri wa anga zinatolewa kati ya Abu Dhabi na maeneo ya Chicago, San Francisco na Washington, D.C pamoja na safari mbili kwa siku New York na mara tatu kwa wiki Dallas/Fort Worth.

 

Kuhusu huduma zinazotolewa kwenye vyumba vya mapumziko vya shirika la ndege la Etihad

Wageni hukaribishwa na wahudumu wenye uzoefu, huwaonyesha mahali wanapotakiwa kuwapo kwa huku wakiwahudumia kwa ukarimu kutokana na mafuzno waliyopata.

Eneo la mapumzikohuandaliwa vyema kwenye chumba maalumu. Mazingira hubadilishwa kila wakati ili kuendanda na madhhari ya Calfonia, Mashariki ya Kati na kwingineko duaniani.

Mlo huandaliwa na timu ya watu wenye mafunzo ya hali ya juu kulingana na mahitaji ya wageni wa eneo husika wanakotoka.

Eneo hilo la mapumziko kwa wateja wa shirika la ndege la Etihad lina mazingira mazuri ikiwamo sehemu za kuchajia simu na huduma zingine za vinywaji.

Kuna menu ambayo imeandaliwa ili kuwapa nafasi wateja kuchagua kile wanachokipenda. Chakula chenye mchanganyiko mbalimbali kinaatikana kwa ajili ya wateja kutoka nchi za latin ambao hupendelea aina Fulani ya chakula kilichotengenezwa kwa ubora zaidi.

 

Kuhusu Fluid Movement

Fluid Movement ilianzishwa mwaka 2009 jijini London ikijihusisha na ushauri ushauri kwenye bidhaa za vinywaji. Lengo lake lilikuwa ni kuleta ufanisi kwenye vinywaji na wafanyakazi wake tofauti na ilivyokuwa hap awali.

 Tangu kipindi hicho imekuwa ikiendesha ushauri, semina na kuandaa mikutano kwenye zaidi ya nchi 30 duniani.

 

KUHUSU SHIRIKA LA ETIHAD

Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad  ni linafanya shughuli zake ulimwenguni kote likifanya shughuli zake; kupitia Shirika la Ndege la Etihad, The National Airline of The United Arab Emirates, Etihad Engineering, Hala Group na Airline Equity Partners.

Shirika limewekeza kwenye mashirika nane; : Airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways, Virgin Australia, na Swiss-based Darwin Airline, inayofanya kazi kama  Etihad Regional.

 

Kwa maelezo zaidi tembelea: www.etihad.com
Makao makuu yake yakiwa Abu Dhabi, Shirika la Etihad limetangaza malengo ya kuhudumia abiria 117 na mizigo Mashariki ya KATI, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Amerika. Shirika lina ndege za Airbus na Boing 122, ikiwa na zingine 204 ambazo bado zinatumika kwa sasa; , ikiwamo  71 Boeing 787s, 25 Boeing 777Xs, 62 Airbus A350s and 10 Airbus A380s

Kwa mawasiliano zaidi;

Tel: +971 50 818 9596

Email: [email protected]

Leave a Comment