Stori: Imelda Mtema, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Staa wa Sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krish’, anadaiwa kuwa kwenye penzi zito na mmoja wa Wakuu wa Mkoa wa Tanzania (jina lipo).
TUJIUNGE NA CHANZO
Habari kutoka kwa chanzo makini cha gazeti hili ambacho ni mtu wa karibu wa Uwoya zilieleza kuwa, staa huyo anadaiwa kumnyakua mkuu huyo wa mkoa (RC) kutoka kwa mwigizaji mwenzake wa Bongo Muvi hivyo kuibua bifu zito kati ya wasanii hao.
WALIANZIA MBALI
Chanzo hicho kilitiririka kuwa, ukaribu wa Uwoya na mkuu huyo wa mkoa wenye changamoto ulianza muda mrefu wakati mwanadada huyo akisaka Ubunge wa Viti Maalum kwa Mkoa wa Tabora kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Hata hivyo, aliikosa nafasi hiyo.
MAMBO YABUMBURUKA
Ilisemekana kwamba, awali mambo yalikwenda kichinichini lakini kadiri siku zilivyosonga ndivyo ishu ilivyoanza kubumburuka ambapo miezi miwili iliyopita ndipo tetesi zikashika kasi.
“Kwa taarifa yenu Irene (Uwoya) amemdatisha ile mbaya ….(anatajwa mkuu huyo wa mkoa) na hiyo ndiyo habari ya mjini kwa sasa.
AMTAJA MTU WA AWALI
“Mwanzoni mkuu wa mkoa alikuwa ni mtu wa….(anatajwa msanii maarufu wa Bongo Muvi) lakini amezima kwa Irene na sasa wapo kwenye mapenzi mazito,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Hata mke wa mkuu wa mkoa ameshashtukia mchezo mzima baada ya kufikishiwa nyepesinyepesi hivyo anachunguza ili amchukulie Irene hatua
kali japokuwa hajasema atakachomfanyia akishanasa ushahidi.”
UWOYA HUYU HAPA
Baada ya kufikishiwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Uwoya na kumbana ambapo kijasho chembamba kilimtoka akiomba ishu hiyo isiende hewani kwani naye alishaisikia kama miezi miwili iliyopita na ikiandikwa itamchafua.
“Mimi mwenyewe nilishangaa niliposikia watu wanadai natembea na ….(anamtaja mkuu huyo wa mkoa) lakini ukweli ni kwamba ni mtu wangu wa karibu ila siyo mpenzi wangu kwani najua ana ndoa yake,” alisema Uwoya kwa kifupi huku akikanusha kuwa na bifu na msanii yeyote wa Bongo Muvi.
MKUU WA MKOA SASA
Kwa upande wake mkuu huyo alipoulizwa kuhusu ishu hiyo aliruka futi mia kwa madai kwamba wasanii wa Bongo Muvi ni kawaida yao kusingiziana mambo kama hayo lakini hayana ukweli.
“Hayo ni mambo yao ya kusingiziana. Sina uhusiano na huyo msanii, hao wasanii nashindwaga hata kuwaelewa, badala wafanye kazi wao kila siku ni kuzushiana tu mambo ya ajabuajabu,” alisema mkuu huyo wa mkoa huku gazeti hili likizama mzigoni kusaka ushahidi wa kutosha ili kuianika ishu hiyo kwa mapana yake.
Kabla ya skendo ya kutoka na mkuu wa mkoa, Uwoya aliwahi kuolewa na msakata kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ kabla ya kudai kutoka na msanii wa Bongo Fleva, Msami Giovanni waliyemwagana hivi karibuni.