×

Waziri Kigwangalla Atoa Saa 24 kwa Polisi Kumkamata Dk. Mwaka

DK+Mwaka+PHOTO

Dk. Juma Mwaka.

NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla leo ametoa saa 24 kwa Jeshi la Polisi kumkamata mmiliki wa kituo cha tiba asilia cha Foreplan, Dk. Juma Mwaka kwa kukiuka amri halali ya serikali ya kusitisha kazi zake.

Dk Kigwangalla

Dk. Hamisi Kigwangalla alipokuwa kwenye kliniki ya Dk. Mwaka. (Picha na Maktaba).

Agizo hilo amelitoa baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kwenye kiliniki hiyo iliyopo Ilala Bungoni jijini Dar, ili kufanya ukaguzi akitaka kujua nini kinachoendelea kwenye kliniki hiyo ambayo hivi sasa imebadilishwa jina na kuwa kampuni.

Ilimlazimu asubiri kupata kibali cha polisi ili kuweza kuingia ndani ya jengo la Dk. Mwaka kufanya ukaguzi huo ambapo amesema amekuta shehena ya dawa za tiba asili licha ya kupigwa marufuku na Baraza la Tiba Asili.

Leave a Comment